World News

Tuesday, May 26, 2015

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA MJINI BREMEN,UJERUMANI JUMAMOSI 30 MAY 2015


FFU Kulitingisha hekalu la UEBERSEE MUSEUM-Bremen,Ujerumani siku 30 May 2015

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band almaarufu kama FFU-Ughaibuni yenye maskani yeke nchini Ujerumani,siku ya jumamosi 30 Mei 2015 bendi hiyo italitingisha hekalu la Uebersee Museum mjini Bremen,kuanzia Saa moja Usiku hadi kumekucha. 
 
Onyesho hilo la usiku usiokwisha limeandaliwa na utawala wa hekalu hilo la makumbusho la Uebersee Museum,ambapo utawala huo umeiomba bendi ya Ngoma Africa band kwenda kutumbuiza,kwa kuwa bendi hiyo ilitumbuiza mwaka 2013 na  kuvunja rekodi ya kuwavuta washabiki wengi kuliko bendi yeyote katika historia ya matamasha yafanyikao katika hekalu hilo.
 
Ngoma Africa band inayoongozwa na kamanda  Ras Makunja ni bendi pekee ya kiafrika yenye mvuto mkubwa barani ulaya,na washabiki wake wameipachika majina mengi ya kiusanii kama vile FFU-Ughaibuni,Viumbe wa ajabu  ANUNNAKI Alien's (himaya ya mazimwi wa Anunnaki), pia maarufu kwa majina kama Mzimu wa Muziki,na "Watoto wa Mbwa" . 
 
Ngoma Africa band pia inatajiri wa wanamuziki wenye vipaji vya hali ya juu wakiwemo yule mpiga solo mahiri Afande  Chris Bakottesa aka Afande Chris-B, Sanjint major Jo jo Sousa, wanamuziki chipukizi wengi walizalishwa na bendi hiyo ambayo inawanamuziki kumi.
 
Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 na kiongozi wa bendi hiyo ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo nyingi za bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja.
unaweza kuwasikiiza FFU

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...