World News

Monday, June 15, 2015

Wapigie KURA DIAMOND & VANESSA TUZO ZA MTV AFRICA 2015

  

Tanzania inawakilishwa na wasanii wawili kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards 2015 (MAMA), ambao ni Diamond Platnumz pamoja na Vanessa Mdee.

Ili Diamond na Vanessa waweze kushinda, nguvu kubwa inahitajika kutoka kwa mashabiki kwa kupiga kura kwa wingi sababu ushindi wa mabalozi hawa wa burudani ni ushindi kwa taifa zima la Tanzania.


Diamond anawania vipengele vitatu ambavyo ni Best Male, Best Collaboration na Best Live.

Upande wa Vanessa anawania kipengele kimoja cha Best Female.

Wasanii wengine wanaoiwakilisha East Africa ktk Tuzo hizo ni SAUT SOL kutoka Kenya.


Njia ya kupiga kura ni moja, ingia kwenye website ya http://mama.mtv.com/voting/ na ufate maelekezo rahisi ya jinsi ya kupiga kura.

Support muziki wa nyumbani ili uweze kufika mbali kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...