Friday, July 3, 2015

Mzimu wa Ngoma Africa band kuibukia Mamling Festival Jumapili 5 Julai 2015-Austria


Mining City,Austria,

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni,yenye makao nchini Ujerumani,inatarijiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni Mamling Festival  siku ya jumapili 5 Julai 2015 alhasiri katika viwanja vya Schlosspark,Mamling 3, Mining nchini Austria. 
Watayarishaji wa onyesho hilo wameitaja bendi hiyo ya Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu unawapeleka puta washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini Austria wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima. Kikosi kazi hiko chenye tabia ya kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki lukuki kote duniani,kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria. Ziara ya bendi hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya wanamuziki wapo katika swaumu lakini watatekeleza wajibu wao.
 
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja ni bendi iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama FFU-Ughaibuni, "Watoto wa Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien' na mengi mengineyo. ni bendi yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbili mpyakatika CD " La Mgambo" za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda .

wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com

No comments:

Post a Comment