Friday, September 11, 2015

LYRICS za ViVa ROMA ViVa!!

Verse I

Nimeshapigwa sana Mkwara na jumbe za Vitisho
ila siamini huu msafara ni vibaraka wa Mrisho
si tulianza sawa vita ya kuitetea Ikulu?
leo umeisaliti UKAWA kwenye sherehe za Uhuru
Uhuru uko wapi mnasherehekea uhuru!?

Uhuru wa kutowafilisi viongozi wakijiuzulu?
Na wanaokufa maskini wanangu wa Burya Nkulu
Mungu aliwapa madini mnambinafsisha Mkaburu!
Bungeni sioni kinachoendelea, naona wasomi wakisutana umbea
wengine walishikwa ugoni picha zilienea
hamuwaoni jimboni afu bado mnawalea
Mambo ya......... spika anabadilisha mada
akiona chama tawala amedhalilishwa kada
Spika wa bunge ona analinda watu wa chama chake
na bunge ni la watu wote sio chombo cha watu wachache

Safari ya Raisi eti tume inaundiwa tume
wakati mwananyamala wanatibu tezi dume
kadi chama nachana nanyongea ganja navuta
nikamateni si mlimshindwa Tibaijuka?
Leta Defender, leta wajeda, leta wagambo Roma nimejitoa sadaka
Na mkitaka kuniua hiki kichwa sifii hapa
nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa

Mother**** walafi wa madaraka
hata Nyerere, Gaddafi si walikufa kwa mashaka?!
So hakuna kiongozi msafi
je nani mwenye mamlaka, anitajie mtoto wa Raisi anayesoma shule ya Kata!


 Chorus
VIVA ROMA VIVA X4
Bendera x3

 
Verse II



Katiba ni sauti ya umma na kuna uhuru wa kuongea
Na nyie si ndio mmenituma, mpo tayari kunitetea?
Wilaya mnafanya mkoa ili wapangwe washkaji
mkuu wa wilaya changudoa hii ni miradi ya upigaji
watasafirisha nyani, sisi tunashangaa Twiga?
utamfunga nani yeye na mwanasheria mkuu ni maswahiba
na wasanii tuombee Rais ajaye asipende tu vikuu
wataalikwa wapemba hatutamuona hata Lukuvi!

Unampigiaje kura fisi awaongoze mbuzi
kwa hongo ndogo ya kipisi unampa ikulu mlanguzi
Geita mlinyimwa dhahabu watawalaghai kwa vitenge
napata ghadhabu propaganda za wabunge wasenge re ma
Ukistaajabu ya Lema utayaona ya Mrema
ona pepo la usaliti linaitafuna Chadema
kwetu Rais ni taasisi inayochaguliwa na mfumo
sisi wawakilishi na kwenye maamuzi hatumo!

Watoto wao wanauza ngada, baba Fisadi, mama anafanya ukahaba
yupi mwema kiitikadi?
Na vita ya mahakama ya kadhi ni uhasama wa wazi
yaani unaisaka bikira ndani ya wodi ya wazazi?
Nipige risasi ya utosi, si ndio nidhamu ya utawala
maana waliomuua Mwangosi waliongezewa mshahara
Doctor Mvungi ona dah!
wakamzawadia jeneza na hawafungwi
Nipe kesi nitaimba ndani ya gereza..

Peperusha bendera

Mbona mama yako anauza gongo na gongo ndio imekulea hadi leo umekuwa polisi
na umpeleki segerea life is not fair
Polisi mnamaisha gani? mnakufa masikini kwa kuwatetea wanyang'anyi!

Chorus
Peperusha bendera
ViVa ROMA ViVa
Bendera x4


verse III

Hakuna mtoto asiye na mzazi yupi wa serikali ya tatu?
mikataba iweke wazi demokrasia ni watu,
ona sasa kila msomi anaikimbilia siasa,
nchi itajengwa na nani? ajira imekuwa serious!

Wanafanya biashara haramu bado hawalipi kodi
nani atahoji na hao ndio wadhamini wa bodi?
Jasho analila mzungu wachimbaji wadogo wa migodi
au mnataka Ivan aje awe mfuasi wa panyaroad?

Pesa starehe za Muungano hamzingatii itifaki
wanafunzi mnawachoma jua na shule hawana madawati
mnalipa mishahara hewa, na hamlipi mafao walimu
na mlimpiga Warioba alivyowaletea Rasimu!

Nchi inalima pamba nyinyi mmeua viwanda
tunauzia wawekezaji ona dola inapanda
Tunageuka waagizaji kisha wanatuuzia mitumba
uchumi unayumba leta fujo upigwe kama Lipumba!
Nakutabiri nani afuate? Karibu Tanga kunani...
Huku hatuitaji kakakuona wala pweza wa ujerumani
Round hii kombe linaenda Monduli?(Masai yelo subhai...
Au kombe ni la Magufuli?
Kama kawa kama dawa, Je kombe linabaki Ukawa?!
Mmarekani anataka wese(we hakuna atakaye pona)
na Mchina akifuata gesi? mwambie Nangwanda sijaona.

Chorus

No comments:

Post a Comment