Thursday, January 7, 2016

MSAKO WAHAMIAJI WANAOCHUKUA AJIRA ZA WAZAWA USIFANYIKE KWA UBAGUZI


WACHINA NA WAZUNGU NAO LAZIMA WASHUGULIKIWE ! BONGO SIYO SHAMBA LA BIBI !

Ni juzi tu naibu waziri wa mambo ya ndani muandisi Mhe.Hamad Masauni aliiagiza Idara ya Uhamiaji kusaka na kuwakamata  raia wageni wote wanaochukua ajira zinazoweza kufanywa na wataanzania, wito huo tayari umeshaitikiwa na idara ya uhamiaji mkoa Dar-es-salaam kama alivyosema Afisa Uhamiaji mkoa Bw.John Msumule kuwa watawasaka wahamiaji wanao chukua ajira za watanzania na kuwafikisha mahakamani.

Mashaka ya ubaguzi katika kamata kamata hiyo! inawezekana zoezi hilo likafanyika kwa
ubaguzi bila makusudi,na wakakamatwa mfano raia wa Somali na wahabeshi wanauza milungi,warundi na wanyarwanda ambao ni wakimbizi, namakundi mengine ambao ndio
vinara wanaoongoza kwa kunyakua ajira zinazowezwa kufanywa na watanzania wakaachwa.
 Mfano katika maeneo ya Kariakoo kuna wachina wanauza maduka na wanamiliki maduka tunajiuliza hivi kweli vibali vya uwekezaji vinatolewa ovyo mpaka
kwa wachina kuwekeza katika maduka?!

WAZUNGU NAO WAMO ! kuna raia wengi wa kizungu wameingia hapa kwa viza za kutalii na sasa wanafanya kazi mpaka za upishi na kutembeza watalii ! sasa inashangaza hii nchi kweli Shamba la Bibi ?

KUNA MADANGULO yenye machangudoa kutoka Asia nayo yasakwe pia

Kuna walinzi makolokoloni raia wa kigeni nao wanavibali vya kuishi na kupata ajira hapa nchini ?!
Leo tunao hapa nchini Wachungaji katika makanisa ! wachungaji hao wengi wao toka Nigeria na makanisa yao yameibuka kama uyoga na kupata vibali vya kuendesha shughuli zao Tanzania! 


Wanenguaji na Marapa katika bendi za muziki nao pia kutoka nje ya nchi! hivi kunengua nako kuwashinde watanzania ?

TUNAIOMBA IDARA YA UHAMIAJI IFUTE NA KUVIHAKIKI VIBALI VYOTE VYA WAGENI

Zoezi hili lazima liwashikirikishe wananchi na serikali za mitaa

Hapa Kazi TU
Na Buberwa.

No comments:

Post a Comment