Monday, May 25, 2009

DULLAYO, OMY G, XDIZO, POMPIN, NA EAZY MAN WAUNDA KUNDI LA MAKAVU LIVE,



Combine ya longtime tu toka kitaa 'Makavu live' inakuja rasmi na tayari jamaa wameshaachia nyimbo inayowatambulisha vizuri tu inayoitwa ONGEA MWANA iliyotayarishwa na producer Vil wa V nice production, studio ambayo ilivamiwa na majambazi siku za hivi karibuni.


Makavu live imeundwa na wasanii 5 wa muziki wa kizazi kipya ambao ni Omary Muba'Omy G', Abraham
Kasembe'Dullayo', Xavier Renne 'Xdizo', Pompin na Isihaka Salehe 'Eazy man'.
Jamaa walikua wanakutana maskani mitaa ya ukonga huko pande za airport wakawa wanachanana kwa ma-freestyle makalimakali ambayo walikua wanayaita makavu, ndipo walipopata familia yao iliyo batizwa jina la makavu live.
Tayari wameshafanya nyimbo nyingi tu za bongofleva mpaka za mnanda zilizotengenezwa na maproducer tofauti hapa jijini. Wanasema " kiparatuni chetu kinatusaidia sana hasa kubadilishana uzoefu katika sanaa kwani kuna wasanii kibao wenye style na skills tofauti tofauti, Mungu atatusaidia familia itakua na tutaibua wasanii wengine wenye vipaji vilivyojificha".
Yupo mwana hiphop mkongwe, Omy G msanii mwenye sauti ya pekee aliyetoka tangu mwaka 2000 na nyimbo ya 'kindumbwendwe'akiwa na kundi la FDC, kwasasa alitoa nyingine inayoitwa 'choo cha kike'kabla ya kuachia 'Skiliza mchumba' aliyomshirikisha Dullayo.

Dullayo a.k.a D-timing anae-shine sana na 'bila yule'
aliomshirikisha Mwana-Fa sasaivi ametoa nyimbo nyingine inayoitwa haya 'makavu live' aliyompa shavu mwanae Joslin walie kuwa wote Mj's record, pia yupo Xdizo alieachia kali yake inayoitwa 'Dhahabu zilizopotea' ikitengenezwa na Marco Chali bila kumsahau Pompin mkali wa freestyle na Eazy man anae-shine sana kwenye nyimbo yao ya mnanda inayoitwa 'maneno wapi'.


Pamoja na kuwa wapo kwenye kundi moja kila msanii yuko huru na anaendelea kusuka albam yake bila kuadhiri muungano wao. Sasaivi wapo katika mchakato wa kutangaza muungano wao, wanapiga picha za pamoja na video za nyimbo zao mpya.

1 comment:

  1. mark.mushi wa italy,aka-mack-mimi ni msanii wa bongo flava ninaishi italy,ninajiandaa kutoka na single yangu inayoitwa-mziki mzuri-jina langu la usanii ni mark.izack wengi mashabiki wangu upenda kuniita mack,kwa kweli jamaa hawa wa makavulive ni kundi ambalo linakuja juu sana kwa kasi ya ajabu kama chelsea footbal club?mko juu kama john terry,mnatisha kama drogba mnadatisha kama ub40,lampard,mark.izack?nawapa pongezi sana kazi zao ni nzuri nimezisikiliza nimezipenda sana ila napenda nione zaidi video zao,pia mungu akipenda kwa kuwa mimi ni msanii ningependa nifanye nao kazi ya mziki siku moja,makavu mpo juu juu zaidi,big up x-dizzo,dullayo,by mack wa italy,nicheki kwenye,chelseaforte1@yahoo.it,au nipigie simu namba+393336989592,ciao

    ReplyDelete