MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Abubakari Mzuri analalamikiwa kumtelekeza mtoto wake wa kike wa miezi minne.
Akiongea na blog hii, mama wa mtoto huyo, Asina Luhura alisema kuwa Mzuri amemtelekeza yeye pamoja na mtoto wake ambapo kwa sasa hatoi huduma ya aina yoyote ambapo mtoto huyo amepewa jina la Khayytham Mzuri.
Alisema kuwa alianza mahusiano ya kimapenzi na Mzuri tangu akiwa shule ya Sekondari ambapo kipindi hicho Mzuri alikuwa msanii katika kundi la Funikas Team lenye maskani yake Ilala.
Asina alisema kuwa Mzuri alimuahidi mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga nae ndoa lakini kipindi alipomueleza kuwa ana ujauzito wake hakuonyesha dalili zozote za kutoa huduma.
Alisema kuwa tangu alipojufungua hata siku moja Mzuri hakuwahi kupeleka matumizi ya aina yoyote ambapo kwa sasa Asina ameshindwa kuendeleza kumnyonyesha mtoto baada ya kupata uvimbe kwenye chuchu kwani anachomwa sindano.
"Mzuri hataki kuleta matumizi ya mtoto ambapo kwa sasa ninapata shida sana kumnunulia maziwa kwani hanyonyi kwa kuwa daktari amenikataza kwani natumia dozi ya sindano ambazo nachomwa katika ziwa hivyo kwa afya ya mtoto nimeambiwa nipumzike kumyonyesha" alisema Asina
"Mie ndio niliyemshauri Mzuri kuingia katika mambo ya kimuziki baada ya kuona kuwa anaweza kutokana na kipaji chake, lakini sasa hivi anakuja kuniacha na kunitelekeza mie na mtoto mchanga kitendo ambacho nashindwa kuelewa hatma ya maisha yangu" amesema Asina
Makavu Live baada ya kumtafuta msanii huyo kwa kipindi kirefu ambapo kwa sasa yupo katika kundi la TOP Band, alisema kuwa mtoto huyo sio wake hivyo hao wanaosema kuwa amemtelekeza mtoto wanataka kumchafulia jina.
"Mie nashangaa kwanza hizo habari ndio nazisikia leo mie sina mtoto kwa sasa hao wanaosema kuwa nimtelekeza mtoto wanataka kuniharibia jina langu" alisema Mzuri.
No comments:
Post a Comment