Friday, June 19, 2009

4NCE B' : WASANII TUSHIRIKIANE, AACHIA NYIMBO YAKE MPYA - " U make me feel so high"

Oscar Alphonce a.k.a 4nce B


MSANII chipukizi wa muziki wa Hip Hop nchini Oscar Alphonce '4nce B' , ametoa wito kwa wasanii nyota nchini wa muziki huo kuweza kushirikiana vyema na chipukizi kwa ajili ya kuwakwamua kimuziki.Akizungumza na blog hili, 4nce alisema kuwa wasanii mbalimbali wa muziki huo ambao wameshavuma na kujipatia umaarufu, wamekuwa wakikataa kushirikishwa katika nyimbo za wasanii chipukizi.


Alisema kuwa kwa sasa ameshaipua kibao chake cha kwanza kinachokwenda kwa jina la You Make Me Feel kilichorekodiwa katika studio ya FIZ RECORD na yeye mwenyewe akishiriki kufanya prodoction, ambacho kimeshaanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.
Alisema kuwa amekamilisha kurekodi nyimbo tano ambazo anatarajia kuziachia hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya albamu yake mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.Alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo anatarajia kuziachia kuwa ni pamoja na Hip Hop, Tusijisahau, Hawapendi, Life Stile na Baby ambazo amezirekodia katika studio ya Fiz chini ya Mtayarishaji wa muziki Fiz.

No comments:

Post a Comment