Monday, June 29, 2009

SHERIA YA HATIMILIKI HAIWASAIDII WASANII TZ - MBUNGE

Mwanzoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Martha Mlata, pichani kushoto amesema kuwa sheria ya mwaka 1999 ya Hatimiliki ya kazi za sanaa haijaweza kutatua tatizo la uharamia wa sanaa na hili limekuwa likiwapatia hasara kubwa wasanii, aliyasema hayo wakati akiuliza swali bungeni.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw Joel Bendera alisema kuwa si kweli kwamba sheria na, 7 ya mwaka 1999 ya haki miliki na haki shirikishi inayohusiana na kazi za sanaa haijaweza kutatua tatizo la uharamia wasanaa ukweli ni kwamba sheria hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo hilohapa nchini.

Alisema kuwa serikali inatambua ukubwa wa biashara ya kazi za sanaa kama vile muziki ambapo biashara ya CD,VCD na DVD inafanyika na ukubwa wa biashara hiyo unatokana nakukua kwa sekta ya utamaduni, kuongezeka kwa wasanii na wapenzi wa muziki na filamu mbalimbali zikiwemo za kitanzania na za nje ya nchi na hivyo kulifanya soko la bidhaa hiyo kuongezeka.

Alisema kuwa jumla ya kodi iliyokusanywa kutokana na biashara ya kazi za sanaa nchini kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi Mei mwaka huu ni shi, 2,086,472,366 bilioni.

Hata hivyo alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi sasa jumla yakesi 8 zinazohusiana na kazi za sanaa zimefikishwa kwenye vyombo vya dola katika mikoa mbalimbali hapa nchini, zote zilisikilizwa na waliopatikana na hatia walitozwa faini ya shs. 20,000 hadi 200,000.

No comments:

Post a Comment