Msanii mahiri wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Kassim Mganga 'Kassim' amekamilisha albamu yake ya2 aliyoipa jina la 'Usiende kwa Mganga' ambayo anatarajia kuingiza sokoni juni 30 mwaka huu.
Akizungumza Dar es salam mchizi alisema albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 10 ambazo amezifanya katika miondoko tofauti huku pia zikitengenezwa katika studio za Big Time chini ya mtararishaji Said Commorion na Metro Studio kwa mkali Allan Mapigo.
Msanii huo aliyewahi kutamba na nyimbo ya 'Haiwezekani' na 'Awena' alisema albamu hiyo itakuwa kali kutokana na mashairi pamoja ujumbe mzito alioutumia katika mashari yake na kwa kuanzia tayari ameachia 'Usiende kwa mganga' ambao unaonekana kuteka hisia za walio wengi.
Ktk albamu hiyo amewashirikisha wasanii wa2 ambao ni Albert Mangwea 'Ngwea' kutoka Chamber Squad na mwanamama Stara Thomas katika wimbo wa Shaka Ondoa.
"Unajua kila msanii anapoaanda albamu yake huwa na malengo fulani sasa mimi katika albamu hii nimeona wasanii wa kuwashirikisha ni wawili, kwa upande wa stara nilikuwa nikimpenda na kumfuatilia toka ningali nasoma na leo nimefanya nae kazi pamoja", alisema.
Alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwemo katika albamu hiyo kuwa ni Sijali, Bianadamu, Shaka Ondoa, Nakupenda na Umebadilika ambapo aliongeza kuwa mashabiki wake wa miondoko ya mapenzi wakae mkao wa kula kutokana na albamu hiyo kusheheni zenye ujumbe mzito.
No comments:
Post a Comment