Monday, June 1, 2009

Uzinduzi wa video za Feisal, Baby Madaha na kampuni ya Pilipili Entertainment


Nilesh Bhatt mkurugenzi wa uzalishaji wa Pilipili Entertainment akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa kampuni hiyo na Video mbili za wanamuziki Feisal na Baby Madaha uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski juzi.


Kushoto Waziri wa Viwanda na Biashara Mama Marry Nagu, Maadam Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchmark Production, Msanii Feisal Ismail na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, ktk picha ya pamoja baada ya uzinduzi.


Kushoto mwanadada Baby Madaha akishambulia jukwaa wakati wa Uzinduzi wa huo .



Wataalamu wa picha na mziki wakiweka mambo sawia katika shughuli hio ya aina yake.


Kulia chini, Adam 'mzee wa vijimambo' kutoka Times akiwa na wadau mbalimbali wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakishuhudia uzinduzi.

Huu ulikua ni uzinduzi wa aina yake, albamu mbili za tofauti kutoka kwa matunda ya BSS 2008 Baby Madaha na Feisal Ismail sambamba na uzinduzi wa kampuni ya Pilipili Entertaiment. Video zimefanyikia India zikiwa na mahadhi na tamaduni kutoka Tanzania na India. Kazi hio wadau, changamoto kwenye mziki wetu wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment