Saturday, June 27, 2009

XDIZO awaimbia waliokufa.

Msanii wa familia ya makavu-live Xdizo amewakumbuka watu kibao
maarufu na wasio maarufu kwa kuwaimbia nyimbo ya hiphop inayoitwa "Dhahabu zilizopotea ".

Anasema kuna watu wengi sana wamekufa halafu hawajaimbiwa, jamaa kawaimbia nakuwatakia walale kwa amani, sio rahisi kuwataja wote kwenye nyimbo ila nyimbo inawawakilisha wote waliotuacha katika hii dunia.


Pata Lyrics: "DHAHABU ZILIZOPOTEA" - XDIZO

verse I;
Walikuwepo mitume na vipindi vikapita
wafuasi wakafuata baada ya mitume kufa
mgawanyiko wa kazi juu ya kuandika habari
vitabu tunavyosoma vimeandikwa histori
alikuwepo Yesu kristo nae pia alikufa
Mohamed akazaliwa nae pia akafuata
u-islam ukatokea waenezaji wazikwa
waumini waliozaliwa dini wakaifundisha
km wakatoriki wanamkumbuka papa
kwa upande wa lutherani kafa martin luther
dhahabu zenye thamani lkn zimepotea
tuliobaki duniani kwa mungu tunawaombea
dunia km njia binadamu tunapita
dunia inavutia binadamu tunakufa
napokosa amri 10 namkumbuka musa
na nnatubu dhambi zangu napotoa dhaka
wamekufa lkn wameacha darasa
dhaka imekua ada wanafunzi twalipa
ila mkiwa pema nasi mnatuombea
dunia inakwenda kasi na siku zinapotea

chorus;


machozi yanilenga ingawa sikupenda
tuliowapenda still weme..... kufa
atuwezi kurudi tena kuwaona kwa macho
labda roho lakini wame.... kufa
kilichokufa hakisimami, akisemi, hakihemi,
tunawaombea lakini wame.... kufa
maproducer waandishi wame... kufa
watangazaji pia wame..... kufa
sisi tunawaombea nyimbo mi nawaimbia
haziwezi kurudi tena dhahabu zilizopotea!!

verse II;

walikuwepo ma-mc wa rnb na hiphop
kipindi walichokufa ukawa mwisho wa kurap
sauti zao kwenye store km ilivyo kwa pac
na memory ya b.i.g skia kwenye hii tack
uwezo wao mwenyezi kawajalia
hapo ulipojenga picha km upo na aaliyah
au lisa lopez lazima utaangusha tearz
na km una roho nyepesi hauwezi kuvumilia
r.i.p niga obd
mungu niepushe na kifo km cha eazy e
sipendi kufa na ukimwi km mi ni mc
sababu ni kioo cha kuelimisha jamii
machozi yananilenga nikiwaza ma-mc
wanathamani lakini wamepotea
km moshi william kwa mungu tunamwombea
kafa james dandu na steve 2k
complex producer km j master j
freak tah nae pia amekufa
fat joe anamkumbuka sana big punisher
mawazo yanajenga picha kwamba utakufa
lkn hayanifanyi nishindwe kujenga future.

chorus

No comments:

Post a Comment