Kampuni ya Double D&G Entertainment imewaandalia tamasha kubwa la muziki wa taarabu wakazi wa Mkuranga mkoani pwani, nje kidogo ya Dsm katika ukumbi wa PARAPANDA HALL ijumaa hii ya tarehe 10/07/2009.
Tamasha hilo limekuwa mahususi kwa wakazi wa Mkuranga na vitongoji vyake, baada ya kukosa show kama hio kwa muda mrefu sana. Ktk onyesho hilo la muziki wa taarab kutakutanishwa vikundi vi3 tofauti vinavyotokea jijini DSM ambavyo ni Dar mordern taarab chini ya Hashim Said (mzee wa malavidavi), Coast modern taarab chini ya Omary Tego na mtambaji hodari wa kike Hadija Kopa.
No comments:
Post a Comment