Thursday, July 9, 2009

KUMUIGIZA MICHAEL JACKSON KUMEMTOA KIMAISHA

msanii Julius Mbele

Kipindi cha nyuma kidogo kuna majamaa waliokuwa wana igiza na kufanya show kama Michael Jackson, matamasha kibao na mashindano ya disko ya kushek kama MJ yalifanyika mengi sana na washindi kupewa zawadi kibao.

Msanii Julius Mbele maarufu kwa jina la Black Texas au Michael Jackson wa Tanzania ameguswa sana na msiba huo hasa kwa sababu mafanikio yake ya kimaisha, kipato chake na kupata marafiki wengi kumetokana na umahiri wake wa kucheza disko kwa miondoko ya Pop akimuiga mfalme wa muziki huo duniani, Michel Jackson.

ndugu za Michael Jackson wakiwa wamebeba jeneza lake

Anasema kifo cha msanii huyo ni pengo kubwa kwake kwa sababu alikuwa akiishi na kupata fedha za kulisha familia yake kwa kutumia jina la Michael Jackson katika maonesho katika kumbi mbalimbali nchini na nje ya nchi ambako alikodiwa kufanya maonesho.
"Nimewahi kukodiwa kwenda kufanya maonesho ya disko nikimwigiza Michael Jackson katika kumbi mbalimbali nchini na nje ya nchi kama Malawi, Msumbiji, Kenya na Uganda ambako ndiko nilipopata fedha za kujengea nyumba na kuanzisha biashara ya baa,".
Anasema alifanikiwa kumuiga kila kitu Michael Jackson hivyo kupata mikataba hapa nchini na nje ya nchi.

Anasema alianza kumuiga Michael Jackson kutoka akiwa shule ya msingi mkoa wa Ruvuma na baada ya kumaliza elimu ya msingi alihamia Dar es Salaam na wazazi wake na ndipo alipoanza kufanya maonesho katika kumbi mbalimbali ambazo ni Lang'ata wa Kinondoni , Lambada wa Keko Magurumbasi ambako alikuwa akionesha shoo na kuanzia hapo alikuwa kivutio katika maonesho ya kumuigiza Michael Jackson.

Alipata mialiko kibao ya nje ktk nchi za Malawi mji wa Lilongwe, mji wa Mzuzu, mji wa Mkata Bay, Msumbiji katika miji ya Lichinga na Nampula. Nchini Kenya alifanya maonesho katika mji wa Mombasa na Jiji la Nairobi wakati Uganda alifanya maonesho Kampala ambako alipata fedha za kutosha.
Anasema nchini Tanzania kulikuwa na wasanii Bosco Cool J, Baucha, Tito Jackson, John Maganga na Saba Jackson ambao walikuwa wakimuiga Michael Jackson.

No comments:

Post a Comment