Karim Omary a.ka K to tha Olright au 'KO' km wadau wengi wanavyomtambua ni Dj mkali na presenter wa redio tokea kitambo, pichani kushoto yuko mbele katikati akiwa sambamba na Afande sele na wasanii wengine.
Jamaa anapigia mzigo kunako redio Kifimbo iliyopo ktk mji mkuu wa Tanzania Dodoma, kabla ya Dodoma mchizi alikuwa Dar akiongoza kipindi cha kijanja cha 'Bongo dot home' ndani ya redio Times Fm pia alikua akisugua mashine ndani ya redio na ma-club kibao jijini Arusha.
Mchizi kawaasa wasanii wa muziki wa kizazi kipya/bongofleva na style zingine za muziki kuto jikita sana Dar es salaam, kwani kuna ma-fans wao kibao mikoani wanakuwa wanawamiss. Kwa kufanya hivyo pia wasanii watakua wanajitangaza zaidi kibiashara na kupiga mkwanja mrefu zaidi ya kukomalia Dar ambako mashabiki ni wale wale wa siku zote.
" Wambie washkaji watimbe Dom, huku mafans kibao mi nipo na ntawapokea fresh " jamaa amesisitizia wasanii kuandaa show mbalimbali mjini Dodoma, na yupo tayari kutoa ushirikiano na wasanii ktk hilo. Aliongeza kuwa “Kama msanii anashindwa kuwawezesha watu wa Dodoma kujua habari zake inakuwa ngumu kwake kuwajulisha walio nje ya nchi” alisema K.O ambaye ndiye msimamizi wa vipindi katika kituo hicho cha Kifimbo Fm.
No comments:
Post a Comment