Thursday, August 27, 2009

KWA AJILI YAKO LYRICS

Hussein Machozi
Ubeti wa kwanza
Najua hiki ndo kipindi ukipendacho,
Najua sasa hivi upo karibu na redio yako,
Labda peke yako au na rafiki zako,
Naomba kidogo ongeza sauti ya radio,
Nachukua nafasi kuongea nawe kwa wimbo huu (uuuh, uuuh, uuuh)
Nimetunga spesho kwa ajili yako mrembo (uuuh,uuuh,uuuh),
Mtangazaji kati ya wimbo usiweke jingo (uuuh,uuuh,uuuh),
Nimetunga maalum kwa mtu aliye single (uuuh, aliye single uuuuh).

Kiitikio
Kwa ajili yako naimba,
Sauti hii sikia, Bw. Daud Majani
Habari hii pokea,
Zingatia mrembo,usipuuze mrembo (2*)
Zingatia aaaah,zingatia aaaah

Ubeti wa pili
Ndani yaroho yangu uko peke yako,
Usihofu mummy hakuna mwenzako,
Nimezaliwa mimi kwa ajili yako,
Naahidi sitotupa penzi lako,
Nimekupa nafasi kubwa ndani ya moyo wangu, uuuh, uuuh,
Kipingamizi hakuna juu yako,uuuh, uuuh, uuuh
Come closer nipunguze mapigo ya myoyo.
Kiitikio;

Ubeti wa tatu
Moyo wangu unatamani sana,
Mimi kuwa na wewe,
acha niseme hadharani kila mtu asikie,
Moyo wangu unatamani sana kuwa na wewe,
Acha niseme hadharani,
kila mtu asikie,
Asali ni tamu baby kwa anayefahamu,
Sogea karibu yangu,
tulia kabisa,
Lala kifuani kwangu,
sinzia kabisa
Kiitikio;

No comments:

Post a Comment