Bi.
Fatma Kange akiongea na wadau wa Sanaakuhusu mfumo maalum wa kimataifa
wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbaliwakati akiwasilisha mada
kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.Kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA GodfreyLebejo na Katibu
Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego.
Na Aristide Kwizela, BASATA
Huenda
kilio cha wasaniijuu ya wizi wa kazi zao kikapungua kama si kufikia
kikomo iwapo wasaniiwataamka na kushirikiana na kampuni ya Global
Standard One (GS1) ambayo imekujana mfumo wa kimataifa wa kutambua na
kudhibiti kazi za Sanaa.
Akizungumza wiki hii kwenyeJukwaa la Sanaa
la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo
Fatma Kange alisema kuwa, mfumo huo wa kuziwekea alama ya utambuzi
yakimataifa (barcode) kazi za wasanii utasaidia kudhibiti uharamia
kwenye sektaya sanaa na kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi.
“Mfumo huu ni wa kimataifa,umekuwa
ukitumika duniani kote miaka 38 iliyopita, hapa kwetu ni mpya kabisa.Ni
mfumo wa kutambua bidhaa halali kwa kuziwekea alama maalum (barcode)
ambayoitazifanya zitambuliwe kimataifa na kutokughushiwa” alisema Bi.
Kange.
Aliongeza kuwa, mfumo huounalenga
kurasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwafanya wasanii kwanza kujisajili
nabaadaye kazi zao kuwekewa alama maalum ambapo sasa watajua idadi
halisi ya nakala(bidhaa za sanaa) walizozalisha, fedha walizoingiza na
zaidi kutazuia kazi zaokuuzwa hovyo mitaani pasipokufuata taratibu.
“Lengo ni kazi za wasaniikutambuliwa
kimataifa, kuuzwa kwenye maduka makubwa na kupewa thamani halisi.Wenzetu
katika nchi zilizoendelea wako mbali katika hili, kazi zao
zinauzwakwenye art stores tu (maduka maalum ya kazi za Sanaa)”
alisisitiza Kange.
Akieleza jinsi Wasaniiwatakavyojiunga, Bi.
Kange alisema kuwa, wako kwenye mikakati ya kuwaelimishaWasanii lakini
akasisitiza kuwa, mfumo huo huendeshwa kwa wasanii wenyewekuridhia na
baadaye kazi zao kuwekewa alama hiyo ambapo hukatwa kiwango kidogosana
cha fedha baada ya kukubaliana na wasanii wote.
fKwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,
Ghonche Materego alisema kuwa, kwa muda mrefu sekta yaSanaa imekuwa
ikichukuliwa kama ya burudani tu kwa hiyo muda umefika wawatanzania
kuichukulia Sanaa kama biashara na kuipa thamani halisi.
“Kwa sasa Sanaa imekubalika, ule wakati wa
kuiona kama burudani tu umepita. Hatuna ujanjalazima tuirasimishe sekta
ya Sanaa” alisisitiza.
Aliwaahidi Wasanii kupitiamashirikisho na
vyama vyao kuwa, kutakuwa na vikao vya mara kwa mara na kampunihii ili
kuona ni kwa kiwango gani suala la udhibiti na utambuzi wa kazi
zaokupitia nembo hii linaweza kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment