In The Congo-Rhyme Like A Girl Feat Nasambu from Zavara on Vimeo.
Zavara hapa.
Nawatambulisha kazi mpya niliyofanikiwa kuipakua siku hizi za karibuni.. Hii kazi ni limbo uitwao In The Congo,
limbo huh unahusisha kundi la Hip Hop tok a new York, Marekani liitwalo
Rhyme Like A Girl wakimshirikisha mwanadada aitwae Nasambu msanii wa
Afrosoul wa California Marekani ambaye ana asili ya kenya. Wimbo huu ni
juhudi za ushirikiano baina ya wasanii na mimi muandaji kujumuika na
jamaa zetu wanaotaabika huko Kongo. Kuna wimbo pamoja na video, pia
viungo vyenye makala kadhaa zilokwisha andikwa kuhusu mradi huu.
In
The Congo video yake ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la
filamu huko Malaysia tarehe 30 ya mwezi wa tano mwaka huu. ulifanyika
uzinduzi rasmi Nairobi kenya wiki iliyopita, video hiyo imeteuliwa pia
kuonyeshwa Zanzibar International film Festival, Salam Kivu tamasha la
filamu huko Kongo mwezi wa saba. Husika kwenye huu mradi kwa kusaidia
kusambaza huu wimbo kwenye mitandao ya jamii na wote mnowasiliana nao,
ujumbe wake ni WITO kwa jamii kulizingatia suala la Kongo na kufanya
kila wawezalo kuondoa jamii ya huko kwenye MAANGAMIZI. Asanteni na
karibuni
No comments:
Post a Comment