'Mkali wa Hiphop' Awapoza Mashabiki wasimzingua Pozi kwa Pozi......! FB
aSANTENI SANA WATU WANGU WA DODOMA KWA MAPOKEZI MLIYONIPA JUZI.ASANTENI SANA KWA SHANGWE ZA KUTOSHA.MUNGU AWABARIKI SANA
NAOMBA NICHUKUE MUDA HUU PIA KULIONGELEA SWALA LA OMY DIMPOZ. JAMANI
MASHABIKI WETU TUNAWAOMBA SANA MUWE MAKINI NA HABARI MNAZOZIPATA
ZIFANYIENI UCHUNGUZI KWANZA. MANENO ALIYOONGEA OMY YALIKUWA NI YA
KAWAIDA SANA TENA ALIYAONGEA JUKWAANI AKIWA ANAKABIDHIWA TUZO YAKE SIKU
YA TUZO ZA KILIMANJARO.ALIONGELEA SWALA LA WASANII KUFA MASIKINI AKIWA
ANAILALAMIKIA SERIKALI NA MAKAMPUNI KUWA HAVITUSAPOT VYA KUTOSHA SISI
WASANII LAKINI TUNAPOKUFA THAMANI YETU INAONEKANA.LAKINI MANENO HAYA
YAMEGEUZWAGEUZWA NA KUONEKANA SUMU KWA HUYU JAMAA.KAMA LEO KAFANYIWA OMY
DIMPOZ KESHO ATAFANYIWA KALA JEREMIAH.KWAHIYO MIMI NAKEMEA SWALA HILI
KWA NGUVU ZANGU ZOTE OMY HAJAMTUSI ALBERT MANGWEA NA HAWEZI KUFANYA
HIVYO KWA SABABU KWANZA OMY SIYO MLEVI.MASHABIKI TUNAWAOMBA SANA
MSIINGILIE SIASA ZA KIMZIKI MZIKI WETU UNA SIASA NYINGI SANA.YANI
UKIKWARUZANA NA MTU HATA KAMA ANA KIBLOG CHAKE UTAKOMA JINSI AMBAVYO
ATAKUANDIKA NA KUKUHARIBIA JINA.POLE SANA OMY, POLENI SANA MASHABIKI WA
OMY.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI BONGO FLEVA.
No comments:
Post a Comment