Nchi
yetu kwa sasa unapoteza ule muelekeo wa AWALI tuliokua nao yaani AMANI. Kila kukicha matukio tofauti tofauti ya kuhatarisha AMANI yetu yanatokea kitu
ambacho kitatupeleka kwenye VITA vya wenyewe kwa wenyewe.
Mimi
kama Rodgers Israel nimeliona hili na kulitazama kwa jicho la tatu ndio maana nimeweza kuwakutanisha wasanii zaidi ya kumi na kuimba wimbo huu wa TUDUMISHE AMANI ili kuikumbusha jamii ya Watanzania na Dunia kwa ujumla kuwa tunapaswa kuilinda AMANI tuliyonayo kwa ajili ya vizazi vijavyo vya nchi yetu.
Ndani
ya wimbo huu wameimba wasanii zaidi ya kumi maarufu kama watoto wa
Paradise ambao ni Chris wa Jano, Soja B, G wa Simon, G fire, Lady Nike, Mass B, Rayswing The Ngada, Yung Omega, Simpoo, Dj A11, Lady Yoo, Joseph Amani na mimi Rodgers.
Wimbo
huu umetengenezwa na Producer Soja B kutoka pande za TVC RECORDS
Kimandolu Jijini
Arusha.
No comments:
Post a Comment