Lucy ktk vazi la Ufukweni |
Kinyanganyiro
cha kumtafuta mnyange wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa
usiku wa ijumaa baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha
mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 13 waliojitokeza.
Nyota
ya mrembo huyo ilianza kuonekana
mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha
mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Yatch club baada ya
kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo
vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watawakilisha mkoa wa mwanza katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment