Monday, August 31, 2009

WASANII WANOGESHA TAMASHA LA KUPIGA VITA MAUAJI YA ALBINO DAR!!

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini wakiongozana na wasanii wenye ulemavu wa ngozi kama Omary Issa pichani juu ambaye aliimba nyimbo mbalimbali za kupiga vita mauaji ya albino, mwishoni mwa wiki walitoa burudani ya aina yake katika kampeni ya kupiga vita mauaji hayo katika tamasha maalum lililofanyika kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni, jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wasanii nyota waliohudhuria katika tamasha hilo ni pamoja na Soggy Dogy 'Hunter', G. Sollo, Mgosi Mkoloni, 'Marlow' na Mrisho Mpoto 'Mjomba'.

Chifu Rumanyika aka Soggy doggy hunter msanii na presenter wa kipindi cha bongofleva Redio Uhuru fm.

Tamasha hilo ambalo lilibeba ujumbe wa "Tuwajali Wenzetu Albino' lilihudhuriwa na umati wa watu wakiongozwa na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Mbunge wa vitu maalum mwenye ulemavu wa ngozi, Mheshimiwa Al-Shaymaa Kwegir alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, hivyo jamii haina budi kulivalia njuga suala hilo ili mauaji hayo yasiweze kuendelea.

No comments:

Post a Comment