World News

Tuesday, September 22, 2009

SHAA kaachia " Mtimanyongo"


Msanii mkali anayekuja kasi mwanadada Sarah Kaisi a.k.a Shaa akiwa amempa shavu mwana-hiphop Langa ameangusha pini jipya linayokwenda kwa jina la “Mtimanyongo”.

Shaa alisema ngoma hiyo imefanyika katika studio za MJ Records chini ya producer mkali Bongo kwasasa Marco Chali.

Shaa ambaye ni mmoja wa wanaowania tuzo za MAMA’S Awards zinazotarajiwa kufanyika jijini Nairobi mwezi ujao alisema yakuwa huo ni ujio wa album yake ambayo siku si nyingi itakuwa sokoni.

“Ni moja ya muendelezo wa nyimbo zangu zilizoko kwenye album yangu ya “Zamu yangu sasa” ambayo ni moto wa kuotea mbali, licha ya hilo bado nasisitiza Watanzania waendelee kunipigia kura mimi na AY ili tuwawakilishe ipasavyo kwenye tuzo za MTV” alisem Shaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...