Thursday, September 10, 2009

Tamasha la muziki wa asili wenye ubunifu kufanyika Dar Okt. 8 hadi 11 Diomond Jubilee

Tamasha la ngoma za ubunifu la Visa 2 Dance litafanyika Oktoba 8 hadi 11 na kushirikisha wasanii kutoka nchi 6 ktk ukumbi wa Diomond VIP hall kwa udhamini wa Vipaji Foundation.
Akizungumza na blog leo Mkurugenzi wa tamasha hilo, Aloyce Makonde alisema tamasha lina lengo la kutambulishaa sanaa ya ngoma za ubunifu kwa jamii.

"Jamii siku zote imezoea kuona sanaa za ngoma za asili lakini sasa tunajaribu kuja na ngoma za ubifinu ambazo zinatokana na ngoma hizo za asaili ya makabila mbalimbali ya duniani,".

“ Visa 2 Dance ni tukio kubwa ambalo litatoa fursa kwa washiriki toka nchi mbalimbali kuonyesha umahiri wao kwa pamoja katika sanaa ya dansi. “ Hii itakuwa nafasi nzuri kwa wasanii wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao kwenye uwanja wa sanaa wa kimataifa na pia kwa wao kujifunza na kubadilishana uzoefu.”


Nchi zitakazo shiriki ktk tamasha ni Tanzania, Kenya, Uganda, Uholanzi, Ujerumani na Afrika Kusini.
Wasanii watakaoiwakilisha Tanzania watatoka ktk vikundi vya Dogo dogo Centre, Lumumba Theatre, Malezi Culture, THT na Temeke Yourth, wapo wasanii 20 ambapo watachujwa na kubaki 10 ambao watakaa kambini chini ya Mkufunzi kutoka Uholanzi, Massimo Morinary kuanzia Septemba 28.

No comments:

Post a Comment