
Alikuwa na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Babra aliyeamka na hisia za
kupiga nyimbo za Busta toka mwanzo wa show mpaka pale mtangazaji mwenzake
Gerald Hando kumuuliza imekuwaje leo aamke na nyimbo za mkali huyo toka kwenye
kundi la Flip Mode na ndipo alipojibu ya kuwa anahisi kama Busta atakuwa jijini
kwenye onyesho hilo, ndipo walipompigia simu Mkurugenzi wao na kulithibitisha hilo.
Busta ambaye ana album tano anatamba na nyimbo kama Dangerous, Gimme Some More and Woo Hah! Pass the Courvoisier, As i come back, na nyingine nyingi anatarajiwa kuangusha bonge la shoo pale Leaderz jijini Dsm.
No comments:
Post a Comment