World News

Wednesday, October 21, 2009

Mapokezi makubwa yanamsubiri Miss Tanzania 2009 'Miriam Gerald' jijini Mwanza kesho...!!!

Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald anatarajia kuondoka jijini kesho tareha 22 na kuelekea mkoani Mwanza kutoa shukrani zake kwa wakazi wa huku kutokana na ushindi alioupata kuanzia Miss Mwanza na sasa Miss Tanzania.
Mrembo anatarajiwa kuondoka na ndege ya shirika la ndega la Tanzania ATC ambao pia ni wadhamini washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2009. Jijini Mwanza Miss Tanzania atapokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza na viongozi wengine wa serikali kabla ya kuelekea mjini ambako atashiriki ktk kazi za jamii alizopangiwa na Kamati ya miss Tanzania Kanda ya ziwa.

Miss Tanzania 2009 'Miriam Gerald' akifurahi na ndugu zake jijini Dar
Ijumaa ya tareha 23 kutakuwepo na hafla maalum jioni kwa ajili ya kuwashukuru wadau mbalimbali wa fani ya urembo, ambapo jumapili oktoba 25 mrembo atarejea jijini kuendelea na maandalizi ya safari yake kuelekea ktk Mashindano ya Miss World ambayo mwaka huu yatafanyikia jijini Johannesburg Afrika ya Kusini tarehe 12 Disemba 2009.
MUNGU MBARIKI MIRIAM GERALD..... MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...