World News

Wednesday, October 21, 2009

VILL awatoa "Wanna Wa Pinda"


KUNDI jipya la muziki wa kizazi kipya la Wana Wa Pinda linaloundwa na wasanii wawili ambao ni Gabriel Alphonce (Gabo) nyuma pichani pamoja na Said Hassan (Side Teacher) mbele, limeipua kibao chao kipya kinachokwenda kwa jina la 'Ujio' kilichorekodiwa katika stuio ya Apex Records ya Dar es Salaam chini ya mtayarishaji wa muziki Vill ambacho kimeanza kufanya vyema katika medani ya muziki huo katika redio mbalimbali nchini.


Wakizungumza na blog hii, Wana wa Pinda ambao chimbuko lao ni Mkoani Rukwa, wamesema kuwa kufanya vyema kwa kibao hicho kumewasukuma kuanza maandalizi ya albamu yao ya kwanza itakayokuwa na nyimbo 10 ambayo itaingia kuingia sokoni mapema mwakani.

Wamesema kuwa katika albam yao wanatarajia kuwashirikisha wasanii mbalimbali ili kuweza
kuchanganya ladha ya muziki huo, ukitaka kuiskiza ngoma yao mpya check hapo juu kwenye PlayList ya Makavu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...