World News

Tuesday, October 20, 2009

Miss East Afrika 2009 Kufanyika Disemba 18... ilikofanyika Miss Tanzania 2009!!!

Mashindano ya Kumtafuta mrembo ktk nchi za Afrika ya Mashariki na kati 2009 yanatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu Dec. 18 ktk ukumbi wa kisasa wa Mlimani City jijini DSM.Mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya pili sasa mwaka huu yatadhaminiwa na Hotel ya Kunduchi Beach & Resort ya jijini DSM na yatashirikisha nchi zipatazo 14 na warembo 28 kushindana tofauti na mwaka jana ziliposhiriki nchi 10 na kutoa washiriki 26.Nchi zitakazoshiriki kutoka ukanda wa Afrika ya Mashariki ni TANZANIA, BURUNDI, RWANDA, KENYA NA UGANDA. ZINGINE NI DJIBOUTI, ERITREA, ETHIOPIA, SOMALIA, PAMOJA NA VISIWA VYA MAURITIUS, COMOROS, RE UNION, MADAGASCAR NA SEYCHELLES.


Mwaka jana mashindano hayo yalifanyikia Bujumbura mji mkuu wa Burundi na mrembo Claudia Niyonzima juu pichani kutoka nchi hiyo kutwaa taji hilo. Burundi walijiunga na jumuiya hii ya Afrika Mashariki mwezi June 2007, wakiwa wenyeji wa mashindano hayo walitwaa taji hilo mbele ya Raisi wao BW. Pierre Nkurunziza.

Miss East Afrika 2009 Claudia Niyonzima akivishwa taji la kwanza kabisa la mashindano hayo yatakayoendelea Disemba mwaka huu nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...