World News

Tuesday, October 20, 2009

Miss Utalii ILALA Novemba 6....

Washiriki wa Miss Utalii Ilala wakiwa ktk picha ya pamoja ambapo sasaivi wapo mazoezini kuelekea ktk kinyang'any'iro chao kinachotegemewa kufanyika ijumaa ya tarehe 6 mwezi Novemba Da West jijini Dar es salaam ( awali yalipangwa oktoba 30).
Temeke tayari walishajipatia mrembo Erica Allan Miss Utalii Tmk 2009 ktk mchuano uliofanyika ukumbi wa City Garden Septemba ya 25 jijini DSM, wakati Kinondoni nao wanajiandaa kumtafuta wa kwao ktk ukumbi wa New Msasani Club mwezi Novemba na washindi wa Wilaya zote za Dar es Salaam watashindana tarehe 21 mwezi wa 11 kumpata mwakilishi wa mkoa.

Mwaka jana mrembo Vaileth Timoth juu pichani kutoka Dar es salaam alifanikiwa kutwaa taji la Miss utalii baada ya kuwabwaga wenzake 20 na kunyakuwa gari mpya aina ya Nissan Premira yenye thamani ya shilingi mil.15 katika kinyang'anyiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa New World Cinema, Mwenge.


Fainal za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika mwezi Disemba...!!!!!No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...