Saturday, October 24, 2009

Wiki ya Mavazi kufanyika Novemba 4 hadi 6 Karimjee DSM...!!













Kwa mara ya pili mfululizo wiki ya mitindo –Swahili Fashion Week (SFW) itafanyika tena jijini Dar Es Salaam na kuwapa wapenda mitindo siku tatu zilizojaa shoo za mitindo za aina mbali mbali.



Dorothy Lubega mmoja wa ma-designer kutoka Uganda





Swahili Fashion week ni siku chache za mitindo ya kisasa yenye mahadhi ya uswahili na vile vile hujumuisha wabunifu wa mavazi wenye vipaji kutoka sehemu mbali mbali nchini, nchi zinazozungumza Kiswahili na nchi nyinginezo. Katika onyesho hilo wabunifu huonyesha kazi za kipekee zenye mahadhi ya kiafrika zikijumuisha, nguo, viatu, mapochi na urembo mwengine.



Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa onyesho hilo la mavazi mwanzilishi wa SFW Mustafa Hassanali ambaye ni mmoja wa wabunifu maarufu nchini alisema mwaka huu Swahili Fashion Week inahamasisha ‘Mitindo kama biashara.’






Christine Mhando designer wa Tanzania





Wiki ya Mitindo ya mwaka huu itajumuisha wabunifu mavazi 14 kutoka mikoa mbali mbali nchini na wabunifu 6 kutoka nje ya nchi na maonyesho hayo ya mavazi yatafanyika tarehe 4 hadi 6 novemba mwaka huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment