World News

Wednesday, October 28, 2009

Savannah Louge yadhamini Miss Utalii Ilala 2009....


Mwandaaji wa Miss Tourism Ilala 2009 Amina Boka kulia na meneja wa Savannah Lucas Paul kushoto wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Savannah Lodge katika Hoteli ya City Paradise wakatika kampuni ya Chicken Hunt ambayo ni kampuni mama ya Savannah Lodge na Kampala Unirvesity ilipotangaza udhamini wa shilingi Milioni 50 kwa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 6 kwenye ukumbi wa Dar West Tabata jijini Dar es salaam.


SAVANNAH LOUNGE tukiwa kama wadau wa sekta ya Utalii,Elimu na utamaduni,tukishirikiana na Kampala International University tawi la Tanzania ,kwa muda mrefu tumekuwa tukifuatilia mwenendo mzima wa mashindano ya urembo nchi,hususani mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania.


Tumegundua na kuridhika kuwa shindano hili ni miongoni mwa mashindano bora na yenye kufanya vizuri zaidi katika bara la Afrika hususani kimataifa,huku kitaifa likiwa lina fanya vizuri sana katika kusaidia juhudi za serikali ya awamu ya nne ya kutangaza na kuhamasisha utalii nchini na kuitangaza Tanzania ,vivutio vya utalii kitaifa na kimataifa,huku wakiwa wanashinda mataji mbalimbali ya dunia na kimataifa kila mwaka tangu kuanzishwa kwake miaka minne liyopita.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...