World News

Monday, January 18, 2010

" Mzee wa Dodo " arudi Msondo.....!

Waimbaji wa bendi ya Msondo music wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es salaam jana Kushoto ni Juma Katundu na Huseni Jumbe.(Picha na msondo)BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music imemludisha kundini mwimbaji wake maili, Huseni Jumbe 'Mzee wa Dodo' baada ya kukaa nje ya bendi hiyo kwa mwaka mzima
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa kundi hilo, Rajabu Mhamila 'Super D'Alisema, wameamua kumrudisha kundini mwimbaji huyo baada ya kukaa viongozi na kukubariana nae na sasa ameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo mpaka sasa tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka uhu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya huna shukrani na kuwa ipo mtaani kwa sasa inauzwa,

Wakati huohuo, bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi tunakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapiri uwa tupo Leaders Club jijini Dar es Salaam


Alisema, sambamba na burudani hizo pia wamejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka uhu mapema kadri iwezekanavyo alisema Mhamila,
Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhulia kuona maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo azihitaji kuadithiwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...