World News

Wednesday, January 27, 2010

Rais wa Indonesia "SBY" aachia album ya 3 "I'm Certain I'll Make It"..!
Rais Susilo Bambang Yudhoyono a.k.a SBY aliyeingia madarakani tangu Nov. 2004 nchini Indonesia ameachia album yake ya tatu hivi karibuni inayokwenda kwa jina la "I'm Certain I'll Make It".

Rais huyo ambaye alianza shughuli za mziki tangu akiwa shule ameshafanya album zingine 2 kabla ya hii mpya aliyoiachia hivi karibuni huku sehemu kubwa ya wadau 75% wakim-support japo viongozi wengi wakiwa hawapendi au kumuonea wivu.

Waziri wake wa vijana na michezo Bw. Andi Mallarangeng amesema mauzo ya album hii yatakukuwa mchango ktk masuala ya elimu na majanga mengine. Pia alizitaja nyimbo za Dr. Susilo ambazo zimewahi kufanya vizuri ambazo zipo ktk maadhi ya R&B na Country, "My Soul was Enlightened that Night," "For You Sweet Child" na "Save Our Planet."


Susilo ni mwanamuziki wa siku nyingi, hata alipokuwa kijana alishiriki ktk bendi ya Gaya Teruna, mwaka 2000 ndipo alipoamua kurudi tena kwenye na kuandika nyimbo nyingi ambapo mwaka 2007 aliachia Album yake ya kwanza iliyoitwa My Longing for You, na mwaka 2009 akaungana na Yockie Suryoprayogo wakaitwa "Yockie and Susilo" na kuaachia album ya pili iliyoitwa Evolusi.

Favourite male artist; Vidi Aldiano

Mara nyingi Susilo ktk miziki yake amekua akiwashirikisha washindi wa Indonesian Idol na favourite male artist ktk MTV Indonesia Music Awards 2009.

Januarisman, Indonesian Idol

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...