World News

Friday, January 8, 2010

REALITY RAPPERS Walilia kutoka 2010..!


WASANII chipukizi, wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Reality Rappers, wamewataka wasanii wakongwe kutoa ushirikiano ili waweze kufikia malengo waliojiwekea.


Akizungumza na globu hii kiongozi wa kundi hilo Jamal Mchina a.k.a Lapa, alisema kuwa baadhi ya wasanii nyota nchini hawana ushirikiano mzuri na wasanii chipukizi kitu ambacho kinawafanya washindwe kufanya vizuri kazi zao.


Alisema kuwa kundi hilo linaundwa na wasanii watatu kutoka katika makundi matatu tofauti lakini wanafanya kazi kama familia moja, yumo Lapa (kundi la Mabwasha linaloongozwa na Afande Selle), Said Ramadhan a.k.a Yanky (kundi la Mitaa Flani) na Juma Salum a.k.a J Mtanga anayetokea East Coast.

Alisema wanatarajia kuingiza sokoni albam yako ya kwanza mapema mwezi Aprili mwaka huu ambayo itakuwa na nyimbo 10 ambapo mpaka sasa wamesashamaliza kurekodi nyimbo saba.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...