World News

Saturday, January 30, 2010

Twenty % kuingiza album yake ya tatu sokoni, mapema mwezi Feb.!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Abbas Hamis a.k.a 20 Percent, anatarajia kuingiza albam yake ya tatu sokoni mapema mwezi Februari mwaka huu.

20 Percent alisema kuwa albam yake itakuwa na jumla ya nyimbo 10 ambazo amezirekodia katika studio mbalimbali nchini, mpaka sasa ameshakamilisha kurekodi nyimbo zote ambapo baadhi ya nyimbo zake zimeshaanza kufanya vizuri katika stesheni mbalimbali za redio nchini.
Baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na Neno la Mwisho, Tamaa Mbaya, Nilikwenda Salama, Usinibembeleze, Malumbano, na Sio Mfano.

Alisema kuwa baada ya kuiingiza albam hiyo sokoni, anatarajia kumalizia kurekodi filamu yake itakayoitwa 20 Percent Furaha ipo Wapi, ambayo inahusu maisha yake pamoja na muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...