World News

Friday, January 29, 2010

Wasanii waungana kuiimbia Kilosa!

Kampuni ya Tongwe Recordz imeungana na watanzania wengine ktk maafa yaliyotokea huko Kilosa mkoani Morogoro kwa kuwaunganisha wasanii wa bongofleva na kutengeneza wimbo mmoja unaowafariji na kuwahamasisha watanzania "Kujitolea kwa moyo mmoja hata kwa kitu kidogo kuwachangia waliokubwa na maafa hayo Kilosa". Nyimbo hio iliyopewa jina la Kilosa ilitambulishwa na kurushwa leo alasiri kupitia kituo cha redio Clouds Fm mishale ya saa 9 na dk 45.

Baadhi ya wasanii walioimba na kuchana ktk nyimbo hio ni pamoja na FID Q, ROMA, PROF JAY, QUICK ROCKA, MRISHO MPOTO, Q. CHIEF, AY, IZZO B, RUBEN, ADAM MCHOMVU na wengine wengi


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...