World News

Friday, January 22, 2010

Zaidi ya masupa-star 100 duniani ndani ya "HOPE FOR HAITI" leo!!

Lile tamasha kubwa la kuchangia pesa kwa ajili ya kusaidia ndugu zetu waliopatwa na tetemeko kubwa la ardhi j4 ya wiki iliyopita huko Haiti (Haiti relief telethon), linategemewa kukutanisha majina makubwa zaidi ya 100 ktk medani ya burudani duniani wakiongozwa na mwigizaji maarufu na mshindi wa tuzo ambae ndie aliyeandaa tamasha hilo Bw. George Clooney.

Tamasha linafanyika sehemu 2 tofauti Los Angel na New York Marekani ambapo Anderson Cooper ataripoti kutoka Haiti na Wyclef Jean ambaye ni mzaliwa wa Haiti ata-host show hio ya New York. Wyclef na watu wake wa Haiti tayari wamekusanya zaidi ya dollar milioni 1 kusaidia tatizo hilo ambapo watu wengi wamekufa na wengine wakiwa mahututi pia zaidi ya watu milioni 2 kupoteza sehemu za kuishi, Angelina Jolie na mpenzi wake Brad Pitt wameahidi kuchangia dollar milioni 1, sambamba na Rais Obama aliye-pledge kutoa dollar milioni 100 km msaada kutoka USA huku Umoja wa Mataifa ume-donate dollar milioni 10.


Music superstars watakao perform ijumaa ya leo ni pamoja na Bono, Bruce Springsteen, Alicia Keys, Jennifer Hudson, Justin Timberlake, Taylor Swift and Rihana, Jay Z, Beyonce, Madonna, Dave Matthews, John Legend, Shakira, Stevie Wonder, Pras na wengine kibao, ma-actor Denzel Washington, Brad Pitt na Leonardo DiCaprio pamoja raisi mstaafu Bill Clinton pia ataudhuria.

Pia event hio itaonyweshwa live na vyombo kibao vya habari vya kimataifa kupitia channel za ABC, CBS, NBC, Fox, the CW, CNN, BET, HBO, MTV, VH1 na CMT.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...