World News

Thursday, February 18, 2010

KILI AWARDS 2010 ITAKUWA YA TOFAUTI...!

Baadhi ya wasanii waliohudhuria ktk uzinduzi wa Kilimanjaro Tanzania Music awards 2010 wakiwa na Bw. George Kavishe ktk picha ya pamoja.

Ufunguzi wa Kilimanjaro Tanzania Music awards 2010 umefanyika leo asubuhi, kwa hafla iliyoanzia mida ya saa 3 mpaka mchana ktk ukumbi wa New World Cinema jijini Dar es salaam.


Launching hio ilihudhuriwa na wasanii, wanahabari na wadau kibao wa sanaa nchini Tanzania, ambapo maelekezo mbalimbali yalitolewa na maofisi kutoka kampuni za Deloitte Touch, BASATA, OnePlus Communications, na TBL ( Wenye kinywaji cha Kilimanjaro beer ambao ndio mpango mzima!)


Bosi wa Kilimanjaro Bw. Kavishe akielezea jambo katika launching hio huku Fina Mango ambaye ni mkurugenzi wa Oneplus comm. akifatilia kwa makini


Kura zitaanza kupigwa tarehe 1 APRIL na washindi wa Kili music awards 2010 watatangazwa tarehe 14 ya mwezi MAY ambapo ndio kitakuwa kilele cha Tuzo hizo..!!


Mkurugenzi wa BASATA Bw. Materego akiwa na maafisa wengine wakifuatilia hafla hiyo kwa makini leo mchana.


Baadhi ya waandamizi wa kampuni ya OnePlus Communication inayoongozwa na Fina Mango (hayupo pichani) ambao ndio walioratibu event hii wakiwa ktk picha ya pamoja


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...