Wednesday, February 24, 2010

NANI MKALI WA TAARAB TANZANIA, Kesho Mango Garden......

Isha Mashauzi

Mpambano wa "Nani mwanamke mkali wa Taarab Tanzania" unategemea kutambulishwa/kuzinduliwa kesho siku ya Alhamisi tarehe 25 February hii ktk ukumbi maarufu wa Mango Garden uliopo Kinondoni jijini Dar es salaam.


Malkia wa Mipasho Tz 'Khadija Kopa

Mchuano huo utaanza kwa kuwakutanisha waimbaji wa kike wapatao wanne au watano ktk jukwaa moja ambao wanatokea ktk vikundi tofauti vya muziki wa Taarab hapa nchini Tanzania. Kuwataja kwa uchache ni malkia wa Taarab Khadija Kopa (TOT), Mwanahawa Ally (Jahaz), Sabaha Salum (Znz), Khadija Yusuf (5star), Isha 'Mashauzi' (Jahaz) na wengine.


Sabaha Salum

Mratibu wa Mpambano huo alisema, Baada ya kuzinduliwa hio kesho pale Mango wapenzi na mashabiki wataendelea kuwasikiza wasanii hao mpaka itakapofanyika Fainali ya mtanange huo siku ya jumapili tarehe 28 March 2010 ktk ukumbi wa Traverntine Hotel uliopo Magomeni, Dar es salaam.

Bi Mwanahawa Ally

Show hio nzima itasindikizwa na kikundi cha JAHAZ MORDEN TAARAB chini ya kiongozi wake Mfalme Mzee Yusuf siku ya kesho Mango Garden na siku ya Fainali tarehe 28/03/2010 pale Traverntine Hotel kwa kiingilio cha Tshs. 5000/=


Tamasha hili la Mpambano wa mwanamke mkali wa Taarab limedhaminiwa na DIDA CLASSIC BOUTIQUE iliyopo Kinondoni Vijana, pia wadhamini wengine wanakaribishwa.

No comments:

Post a Comment