World News

Thursday, February 4, 2010

Raila Odinga ampigia simu Gordon Brown ili McDonald Mariga asajiliwe Man City..!
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amempigia simu waziri mkuu wa Uingereza Bw.Gordon Brown ili mchezaji wa Kenya McDonald Mariga ajiunge na klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi ya Uingereza kwa dau la £7million kama walivyokubaliana na Parma F.C ya Ital hapo awali.

Kenya ingejivunia sana mchezaji wao kuchezea ligi kubwa duniani lakini panel yenye mamlaka ya kutoa vibali vya kazi Uingereza ilimzuia mchezaji huyo na kumnyima kuchezea Man City, ambapo Inter Milan walijitokeza na kumnyakua mchezaji huyo aliyesaini kuchezea klabu hiyo ya Italia kwa miaka minne.

Jose Mourinho amefurahia kumnunua kiungo huyo ili kuziba pengo la Patrick Vieira ambae nae amekimbilia Ligi kuu ya Uingereza.

Hivyo mpaka sasa hakuna mchezaji kutoka Kenya wala Tanzania ambaye anacheza mpira wa kulipwa ktk ligi kuu ya England, rekodi za karibuni zinaonyesha Savio Nsereko mzaliwa wa Uganda aliichezea WestHam United mechi km 10 hivi tangu tarehe 26 jan. 2009 hadi alipochukuliwa kwa mkopo na Bologna F.C. ya Italia!!!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...