Thursday, April 22, 2010

Dullayo atoka na Kiduku...!


Akiwa ktk maandalizi ya mwisho ya Album yake ya pili Dullayo amesema anaachia ngoma yake nyingine inayofanana sana na ile mipigo ya Ki-Nigeria ambayo ameifanya kwenye studio za Emotion records chini ya producer Kisaka amesema ameamua kufanya hivyo ili kuja tofauti na watu walivyomzoea kwa staili ya nyimbo zake.


Amesema ni nyimbo ambayo mtu uwezi kukaa ikipigwa hasa ni rahisi zaidi kucheza ktk ile staili iliyoingia ya Kiduku, noma mzaz..........


Kwa mujibu wa kauli zake amesema atatoa Hits baada ya Hits, namaanisha kila ngoma atakayoitoa watu watakua hawakai na amebakisha nyimbo mbili tu kukamilisha album yake hiyo ambayo ameifanya ktk studio tofauti tofauti ambazo ni

Emotion Records ambayo ilimfanyia nyimbo yake Naumia Roho,

Studio 69 alikofanya collabo mbili moja na Mr. Blue, na nyingine na QJ,

nyingine ni G Records na Prodyuza KGT,

V Nice Production chini ya Prodyuza Villy, kuna nyingine alifanya collabo na Black Rhino, na mkono mwingine na D Knob, pia amegonga mikono mingine na Prodyuza Jonas yule alifanya Perfume ya Joslin.


Kwahiyo mdau tegemea BONGE LA ALBUM ambalo mpaka sasa mwenyewe hajui aiite jina gani????


No comments:

Post a Comment