
J.Martins msanii mkali tokea pande za Nigeria jana alitua ndani ya Bongo na kufanya bonge moja la show kwa takriban dakika 45 hivi

Show ilifanyika ktk viwanja vya makao makuu ya Zain Tanzania pale Morocco ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kuzidua ile huduma ya Zain ya "UHURU WA KUONGEA"

J alipiga ngoma kama 4 hivi mfululizo na kuwaacha kinadada hoi huku kila mmoja akitaka japo kumshika kidogo tu msanii huyo aliyewabamba mashabiki kibao ndani ya Bongo

ukiachilia nyimbo yake ya Oyoyo inayobengisha vilivyo, mchizi pia aliimba Good or Bad, So Fly na Cool Tamper

Sehemu ya umati uliohudhuria show hio
No comments:
Post a Comment