Tuesday, April 20, 2010

KAKA HAMISI MSANGI WA REDIO TIMES ALIPOUAGA UKAPERA....!



Mwisho wa wiki hii, mfanyakazi wa kituo cha Redio Times Fm Hamisi Msangi na mkewe Salma binti Seleman waliuaga ukapera. Sherehe kubwa iliyofana ilifanyika nyumbani kwa Bw. Msangi pande za Mtoni kijichi jijini Dar es salaam. Hongera kaka...!!


Hamisi na mpambe ambaye ni kaka yake wakiingia ukweni kwenda kujichukulia jiko lao...



Braza kama anamnongoneza hivi, 'dogo usiogope huo ndio ukubwa...'




Shekhe akimfungisha ndoa Bw. Msangi mbele ya mashuhuda kibao, na ubani kwa ukiwabariki kimtindo kwa pembeni




Hamisi Msangi akisaini cheti cha ndoa kwa umakini, huku mzee wake akichungulia kuhakikisha kama kweli kijana kasaini, asije kukimbia!




Bwana na Bibi Hamisi Msangi wakivalishana pete za ndoa baada ya tukio zima kukamilika




Wenye furaha kabisa usoni huku wakiwa wameshikilia na kuzibisu zawadi zao muhimu kuliko zote duniani walizokabidhiwa siku hio


Mzee wa kuhondomola aka mzee wa chakula cha usiku Amani Misana akimpa big-up kijana kwa kuchagua chemaa!
Amri Massare aka Maximo mtangazaji wa kipindi cha viwanjani na mdau mkuu wa globu ya viwanjani hakuwa nyuma ktk kumsapoti Msangi, ila bado yeye sasaaa!!!!

TUNAWATAKIA KILA LAKHERI KTK MAISHA YENU YA NDOA

NA SISI VIJANA WENZENU TUTAIGA MFANO WENU

INSHAALAH!!!


No comments:

Post a Comment