Thursday, June 17, 2010

BASATA yawaasa wananchi kutowabeza Wasanii...!


BASATA imewataka wananchi kutambua mchango wa Wasanii na sivyema kuwabeza kwa kuwaita majina ambayo yanaidhalilisha fani hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na mtoa mada aliyealikwa na Baraza hilo Vicensia Shule,jana alipokuwa akiongea na baadhi ya wasanii na wanahabari katika ukumbi wa Basata.

Shule alisema wasanii wa Tanzania wanajitahidi kwa kiasi kikubwa katika kuielimisha jamii ya Kitanzania kuwa macho katika kitu falani kiwe kibaya au kizuri kwa faida ya Taifa lakini si rahisi kwawao kuipotosha jamii ambayo nao inawazunguka.

"Kwa upande wangu mimi siamini kama kweli msanii wa Tanzania anaweza kuipotosha jamii ambayo inamzunguka kwa sababu msanii kazi yake kubwa ni kuielimisha jamii kuwa makini na jambo fulani ili kutokana na lugha anayokuwa ametumia msanii yenye mafumbo ndiyo watu wanadhani msanii anaipotosha jamii au kupotoka kimaaadili,"alisema Shule.

Shule alisema msanii anatumia sanaa yake kama mawasiliano na hutimia tungo anzo zitunga kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jaminii na ameitaka jamii kuwa makini kwa ajili ya kusikiliza tungo hizo.

No comments:

Post a Comment