Monday, July 12, 2010

Waasi wa Somalia 'Al Shabaab' washukiwa kuua watu 64 wakiangalia Fainali ya Kombe la Dunia Uganda...!

mama akilia kwa uchungu karibu na mwili wa ndugu yake aliyefariki ktk shambulio hilo.


Watu 64 wamekufa papohapo na wengine kujeruhiwa wakati wakiangalia mechi ya fainali ya kombe la dunia kupitia Tv ktk mgahawa wa Ethiopia huko Kabalagala, karibu kabisa na Kampala. Vifo hivyo vilitokea baada ya wanaosadikiwa kuwa waasi wa kikundi cha al-Shabab cha Somalia kulipua mabomu wawili. Al - Shabab wanaonolewa na kupewa mafunzo na maaskari wastaafu kutokea Afghan, Pakistan, na Iraq wapo chini ya Al Qaeda, bomu lingine walilipua Kyadondo Rugby Club iliyopo Nakawa ambapo pia watu walikuwa waki-chek fainali hiyo kati ya Spain na Uholanzi usiku wa jana.


Inasemekana magaidi hao walikuwa wakiwalenga Wamarekani, waEthiopia na Uganda, serikali za Marekani (kupitia kwa waziri wake Bi. Hillary Clinton) na Uganda zimetoa pole kwa waathirika wote

“I join President Obama in strongly condemning today’s attacks in Kampala, Uganda targeting innocent spectators watching the World Cup final,” Clinton said. “We understand that American citizens may have been injured or killed and our embassy is reaching out to assist. Our condolences go out to the families and friends of the victims, in the United States and Uganda.”

sehemu moja ya umati wa wa-Tanzania wakifuatilia fainali hiyo jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment