SHIRIKISHO la wasanii Tanzania (SHIWATA) limeshangazwa na baadhi ya viongozi wa wilaya kupinga mikakati ya kutafuta mashamba kuitikia wito wa Sera ya Taifa wa Kilimo Kwanza. 
Mwenyekiti wa SHIWATA, Bw. Cassim Taalib akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema nia ya shirikisho hilo ni kuwakusanya wasanii kuwa pamoja na kulima shamba la pamoja katika vijiji ambavyo watakaribishwa na vyenye maeneo ambayo yako wazi.
"Wasanii ni masikini,tumeamua kujikusanya pamoja kujenga nguvu imara ya kutafuta shamba la pamoja na kuweka makazi kwa ajili ya kulima vyakula vitakavyosaidia familia zetu na watanzania.Alisema anashangaa kusikia taarifa za kunyimwa ardhi hiyo ambayo wameinunua kwa fedha halali kupitia benki zilizotakiwa na vijiji husika na kufuata taratibu za kujiunga na vijiji.
Alisema hata hivyo Shiwata ilinunua eneo jingine katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ekari 153.05 na kununua shamba jingine la ekari 229 ambazo zitatumika kwa kilimo Kwanza.Bw.Cassian alisema kutokana na mkanganyiko uliojitokeza katika vyombo vya habari, ameitisha mkutano wa wanachama wote Agosti 28 kufafanua jambo hilo. 
Alisema nia ya kuanzisha kijiji cha pamoja cha wasanii umetokana na wito wa Serikali wa kila mtanzania kuanzisha mikakati ya Kilimo Kwanza kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
"Tulijipanga kuhamia Kisarawe tulime muhogo na mazao ya mboga mboga kwa wingi ili tulishe mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar"alisema Bw. Cassian.
Hivi karibuni viongozi wa wilaya za Kisarawe na Mkuranga walikaririwa na vyombo vya habari wakisema hakuna maeneo kwa ajili ya wasanii katika wilaya zao.

"Kwa mfano kijiji cha Visegese,Kisarawe tuliandika barua ya kujiunga na kijiji,tukakubaliwa na kulipa ada ya sh.mil.4.5 ambazo kila msanii alitoa sh. 10,000 ya kujiunga na kijiji lakini hatujapewa eneo hilo mpaka sasa"alisema Bw. Cassim.
Alisema hata hivyo Shiwata ilinunua eneo jingine katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ekari 153.05 na kununua shamba jingine la ekari 229 ambazo zitatumika kwa kilimo Kwanza.Bw.Cassian alisema kutokana na mkanganyiko uliojitokeza katika vyombo vya habari, ameitisha mkutano wa wanachama wote Agosti 28 kufafanua jambo hilo.

Alisema nia ya kuanzisha kijiji cha pamoja cha wasanii umetokana na wito wa Serikali wa kila mtanzania kuanzisha mikakati ya Kilimo Kwanza kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
"Tulijipanga kuhamia Kisarawe tulime muhogo na mazao ya mboga mboga kwa wingi ili tulishe mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar"alisema Bw. Cassian.
Hivi karibuni viongozi wa wilaya za Kisarawe na Mkuranga walikaririwa na vyombo vya habari wakisema hakuna maeneo kwa ajili ya wasanii katika wilaya zao.
No comments:
Post a Comment