Nasaha hizo zimetolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Sekta binafsi, Ester Mkwizu wakati akimkabidhi bendera ya Taifa mrembo huyo tayari kwa safari ya kuelekea China kwenye mashindano ya Dunia ya Urembo ya 'Miss World'.
Ginevieve anatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini China kwa ajili ya Mashindano ya Miss World yatakayofanyika Oktoba 31 mwaka huu, na kushirikisha zaidi ya warembo 120 kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo jana mrembo huyo aliagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Herman Mwansoko na MKurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel Olenaiko pamoja na viongozi mbalimbali.
"Ginevieve unakwenda kubeba dhamana ya nchi, nenda kifua mbele ukiwa unatoka kwenye nchi ya amani na ulinde heshima yako pamoja na heshima ya nchi yako hapo utafanikiwa, na sisi wanzania tunakuombea dua uweze kutwaa taji la Dunia,"alisema Mkwizu.
Naye Ginevieve amewataka watanzania kuondoa hofu juu yake na kwamba hatotishika na wapinzani wake kutokana na maandalizi mazuri ya kisaikolojia aliyoyapata kutoka kwa walezi wake wa Kamati ya Miss Tanzania.
"Nawatoa hofu watanzania ingawa nitashindana na warembo zaidi ya 120 kamwe sitatishika nao, nimeandaliwa vizuri kisaikolojia,"alisema Ginevieve.
Alisema kutokana na fursa hiyo na dhamana aliyopewa na Taifa atahakikisha anatangaza vivutio vya Tanzania kupitia kwa warembo wenzie kutoka nchi mbalimbali pamoja na sekta zote zilizopo nchini.
"kupitia upande wa siasa nitaitangaza Tanzania hasa amani iliyopo na fursa hii nitaitumia bila uoga nawaomba tu watanzania waniombee dua kwani ninajiamini na ninaimani taji la Miss World litatua nchini,"alisema Ginevieve.
Mrembo huyo ataondoka kesho na ndege ya Qatar air kwa ajili ya kambi ya Miss World itakayoanza Oktoba mosi mwaka huu na safari yake itapitia Mongolia ambapo atakaa kwa muda wa siku tatu na baada ya hapo atakwenda Shangai ambako pia atakaa kwa siku tatu kisha ataelekea China kabla ya kutua Kusini Sanya kwa mashindano hayo.
Mrembo huyo ni wa 17 kushiriki mashindano ya Miss World tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Miss Tanzania 1994 ambapo watanzania wanategemea makubwa kutoka kwake kwa kua ameandaliwa vizuri na walezi wake Kamati ya Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment