Wednesday, September 29, 2010

Msondo wawaaga shabiki zao, kukutana tena wiki ijayo TCC Changombe kiingilio buku 2, Max Bar buku 5...!

Msondo ngoma wameondoka jijini Dar es Salaam leo kwa ziara ya maonesho ma5 katika mikoa ya kusini kuanzia Oktoba mosi mwaka huu, baada ya kukaa muda mrefu bila kutembelea kanda hiyo.

Akizungumza jijini Dar leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' (pichani)amesema kuwa ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuitamulisha albamu yao mpya ya Huna Shukrani.


"Tukiwa huko tutafanya kazi ya kuwapa burudani na wapenzi wetu watapata nafasi
ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao kama hayo niliyoyasema.," alisema Mhamila.

Amesema kuwa wataanzia kuangusha burudani ya aian yake katika ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba mosi, ambapo oktoba 2 watakuwa Brantare Hall na oktoba 3 watakuwa katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 watakuwa Nyongoro Hall, Ruangwa.

SUPER D amesema kuwa mbali na utambulisho wa albamu hiyo, bendi hiyo pia itatoa fursa kwa wapenzi wake wa mikoa hiyo kwa lengo la kusikilizishwa vibao vipya ikiwemo Dawa ya deni kulipa na Lipi Jema vilivyoimbwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga.
Pia Mzee Gurumo alitangaza kwenye maonyesho yao mwishoni mwa wiki kuwa wanaelekea kusini, hivo tutaonana nao tena wikiendi ya wiki ijayoooooo

No comments:

Post a Comment