Zantel Tanzania imedhamini tamasha la muziki Afrika Mashariki East African Bash, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye Ukumbi wa Dar West Parck Dar es Salaam. Ofisa Uhusiano wa Zantel, Ikechukwu Kalu alisema wameamua kudhamini onesho hilo, ili kuweza kuwapatia burudani nzuri wadau na wateja wao.
Alisema kupitia tamasha hilo, Watanzania watapata fursa ya kucheza muziki wa wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki.Ofisa huyo alisema tamasha hilo pia litafanyika Jumamosi kwenye ufukwe wa Mbalamwezi Club uliopo Mikocheni Dar es Salaam,wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo kuwa ni Amani wa Kenya, Ngoni wa Uganda pamoja na Ambwene Yesaya 'AY' wa Tanzania.
“Tumeamua kudhamini tamasha la East African Bash kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu burudani safi ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha wasanii mbalimbali,” alisema Kalu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya GLITZ, ambao ndiyo waratibu wa East African Bash, Dennis Busulwa 'Ssebo' alisema tamasha hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa kukutanisha wasanii kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, wadhamini wengine wa tamasha hilo ni Africa Media Group, Air Uganda pamoja na Paradise City Hotel.

No comments:
Post a Comment