Monday, October 11, 2010

Baada ya kupitia ANGAZA, Baghdad ataki tena demu....!

Baghdad punguza kula......

Inatokeaga ukajikuta umepita sehemu mbaya na kuwa na wasiwasi kama inawezekana ukawa umeambukizwa virusi vya HIV, pia imeshawahi kunitokea.........
ndio mambo yaliyomkuta mkali wa Hiphop Baghdad aka G U C C I BOY kwa jinsi alivyonisimulia kdg, imemchukua miezi kama minane hivi tangu hio ishu ilivyomtokea na hivi juzi ndipo akaamua kwenda ANGAZA kwa wale majamaa wanaotoaga ushauri nasaha na kupima km umeambukizwa au lahka!

Blog ya Makavu inampa hongera Baghdad kwa ujasiri alioufanya, maana amepima na kupewa majibu yake yaliyoonyesha kuwa yuko salama kabisa yaani HIV -VE!
ameongeza kusema kuwa kwa sasa yuko SINGLE na hataki demu, ana miaka chini ya 20, uzito wake ni kilo 135.5 na size ya kiuno chake ni 47... du namkumbuka Big Poppa!

Bagdad ametoka kuachia remix ya collabo ya AIR PLANE ambayo awali ilifanywa na wasanii wa Marekani B.O.B na EMINEM na sasa wameingiza maujanja yao yeye, Young Dee chini ya usimamizi wa Tudd ndani ya Ngoma record- goma linapendwa zaid sasaivi na kufanya vizuri ktk chati za redio bongo... Unaweza kuiskiza hio ngoma ipo ktk Playlist ya Makavulive hapo juu kulia.

Pia unaweza kumnyaga live ktk kipindi cha CLUB 10, Radio CLOUDS Fm saa 4 mpaka 6 kila jumamosi!!!!

No comments:

Post a Comment